Bima ya nyumba

1. Nini Maana ya Bima ya Nyumba

Bima ya nyumba inatoa ulinzi kwa nyumba, vitu vya ndani na mali binafsi za familia dhidi ya majanga kama vile moto na majanga yanayoambatana na moto(vimbunga, mafuriko, tetemeko n.k), wizi na hasara zisizozuilika.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara:

2. Nani anapaswa kuchuka bima hii?

Bima hii inaweza kuchukuliwa na mwenye nyumba au mpangaji wa nyumba.

3.Gharama za Bima

Ada ya bima ni 0.15% ya thamani ya jengo. 0.75% Ulinzi kwa nyumba na mali zako kwa Vitu vya ndani. 2% kwa Vitu binafsi vya familia

4.Gharama za Bima

Ada ya bima ni 0.15% ya thamani ya jengo. 0.75% Ulinzi kwa nyumba na mali zako kwa Vitu vya ndani. 2% kwa Vitu binafsi vya familia

5.Nini faida za Bima ya Nyumba?

1.Inakufanya uendelee kiuchumi ukipatwa na janga lolote la mkataba 2.Inakufanya uwe na Amani wakati wote 3.Kinga dhidi ya madai ya kisheria 4.Ulinzi kwa nyumba na mali zako

6.lazima kuchukua bima kwa pamoja?

Sio lazima kuchukua bima hii kwa pamoja. Mfano mwenyenyumba anaweza kukatia jengo peke yake.
Mpangaji anaweza kukatia Vitu vyake vya ndani peke yake.

7.Ni vitu gani unaweza kukatia bima?

Jengo na vitu visivyohamishika katika jengo Vitu vya ndani mfano Runinga, radio,jokofu, sofa, vitanda n.k Vitu binafsi vya familia mfano simu, laptop, vito vya thamani n.k

8.Bima hii inatolewa kwa muda gani

Bima hii inatolewa kwa kipindi cha mwaka mzima