Bima ya kilimo

Nini maana ya bima ya kilimo?

Ni kinga dhidi ya uharibifu wa mazao yako shambani kutokana na majanga mbalimbali kama vile, ukame, mafuriko, kimbunga , wizi , tetemeko la ardhi na uharibifu wa mimea/ mazao kutokana na wadudu wasizuilika kama vile nzige.


Nini faida za bima hii kwa mkulima?

 • Inamfanya awe na amani na mazao yake yakiwa shambani.
 • Inamfanya aendelee mbele kiuchumi hata kama atapatwa na janga Iolote liliopo ndani ya mkataba.
 • Inamsaidia kuongea uzalishaji maradufu kutokana na ushauri atakaopata kutoka kwa mshauri wetu wa kilimo.
 • Inampa uhuru wa kuwekeza zaidi maana hatahofia hasara itokanayo na majanga.
 • Gharama zake ni nafuu.
 • Fidia wakati wa madai ni chapuchapu.
 • Anapata fàida ya gharama za uzalishaji na uharibifu wa mazao unapotokea.
 • Anapata ushauri wa kitaalam kuhusu kilimo wakati wote wa msimu wa kilimo.
 • Inamuwezesha kupata mkopo benki.

Vitu vya aina gani mkulima anatakiwa kukatia bima?

 • Gharama za uzalishaji kama vile mbegu, mbolea, vibarua nk.
 • Gharama za uharibifu wa mimea/ mazao yakiwa shambani.
 • Nyumba na mali zilizomo ndani.
 • Vyombo vya moto kama vile matrekta, gari ndogo na kubwa, pikipiki nk.
 • Mazao yake kuyatoa shambani na yakiwa katika ghala baada ya kuvunwa.
 • Wafanyakazi pamoja na mwajiri/ mkulima.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Nani anapaswa kuchukua bima hii?

Ni mkulima au kikundi cha wakulima kikiwa kwenye kilimo cha mkataba.

Bima hii inatolewa na kampuni gani?

Bima hii inatolewa na kampuni ya Madam pesa microfinance Ltd.

Lazima kuchukua bima ya kwa pamoja?

Sio lazima kuchukua bima kwa pamoja, mkulima anaweza kuchukua bima kwa vipande.

Bima hii inatolewa kwa muda gani?

Inatolewa kwanzia msimu wa kupanda hadi msimu wa kuvuna mazao

Nani anapaswa kuchukua bima hii

Lengo la bima hii ni kuondoa au kupunguza hasara za mkulima ambazo anaweza kuzipata kutokana na majanga mbalimbali kama yalivyo ainishwa hapo juu.